Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam waandaa silaha za maangamizi kuimaliza Simba Nusu Fainali

Dube Dube Prince Prince Dube

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wawili ndani ya kikosi cha Azam FC kwenye safu ya ushambuliaji, Idris Mbombo na Prince Dube wanaandaliwa kuimaliza Simba SC kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Ikumbukwe kwamba Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala ilitinga hatua ya Nusu Fainali kwa kuwatungua mabao 2-0 Mtibwa Sugar na Simba SC ilitinga hatua ya Nusu Fainali kwa kuitungua mabao 5-1 Ihefu mechi zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo uliopita wa Azam FC kwenye ligi ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Jamhuri ukisoma Ruvu Shooting 1-3 Azam FC huku wafungaji wakiwa ni Ayoub Lyanga aliyefunga mabao mawili na Sopu alitupia bao moja. Raphael Varane amfikirisha Erik ten Hag

Washambuliaji Mbombo na Dube walitoa pasi mojamoja za mabao kwenye mchezo huo jambo lililompa furaha Ongala.

Ongala amesema: “Dube na Mbombo hawa wote ni wachezaji wazuri na mechi ijayo ni dhidi ya Simba tunaamini kwamba yule atakayepewa nafasi ataonyesha uwezo wake.”

Simba SC na Azam FC zitakutana Mei 6 katika Uwanja wa Uwanja wa Nangwanda, Mtwara katika Nusu Fainali ya Kwanza ya ASFC huku Nusu Fainali ya pili ikitarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa CCM Liti mjini Singida kati ya Singida Big Stars dhidi ya Young Africans Mei 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live