Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam vs Yanga ni mechi ya kibingwa na ufundi mwingi

Vita Vita Yanga Vs Azam Azam vs Yanga ni mechi ya kibingwa na ufundi mwingi

Sat, 16 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukisikia mechi dume ndo hii. Ni mechi ya lawama vilevile. Lakini kama utapenda kuiita mechi ya kibingwa pia hautakosea, wakati watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, kesho Jumapili watakapokuwa wageni wa Azam FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga ndio mabingwa waliotwaa mara nyingi taji la Ligi Kuu ikifanya hivyo mara 29, wakati Azam ni moja ya timu zilizotwaa mara moja msimu wa 2013-2014 na msimu huu imeonekana kupania licha ya kwamba katika mechi za karibuni ilidondosha pointi nyingine zilizowaengua kileleni mwa msimamo.

Mechi ya kesho itakuwa ni mechi ya mwisho ya Ligi Kuu kabla ya ligi hiyo haijasimama kupisha mechi za kimataifa kwa timu za taifa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na mashabiki wameitolea macho kutaka kujua nani ataibuka na ushindi baada ya kelele na tambo nyingi nje ya uwanja.

Kwa namna ratiba ilivyowekwa ni kama vile leo mashabiki wa soka wameachiwa muda wa kuijadili mechi hiyo ya 32 baina ya timu hizo kukutana katika Ligi Kuu tangu 2008 kabla ya kesho kuishuhudia mara baada ya watu kutoka kupata futari pamoja na chakula cha jioni.

Kwa wale ambao hawatabahatika kwenda Kwa Mkapa wataishia kukaa katika sebule zao au kuibukia vibanda umiza ili kushuhudia mtanange huo, ikizangitiwa kuwa Yanga na Azam haijawahi kuwa mechi ndogo.

Awali mechi hii ilikuwa ipigwe Uwanja wa Azam Complex, kuanzia saa 1:00 usiku, lakini ikahamishiwa Kwa Mkapa na kubadilishiwa muda vile vile hadi saa 2:30 usiku ili kuwapa wasaa mashabiki wanaoendelea na mfungo wa mwezi wa Ramadhani na Kwaresima kufuturu kabisa ndipo waibukue uwanjani kucheki shoo kali. VITA TATU TOFAUTI Mechi ya kesho imegawanyika katika maeneo matatu tofauti - kwanza upinzani na ushindani mkali uliopo baina ya timu hizo, lakini ni ya kutoa dira ya ubingwa kwa msimu huu, huku ikiwa mechi ya vita ya mastaa wa timu hizo wanaochuana kwenye kuwania tuzo mbalimbali za ligi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live