Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam uso kwa uso na Coastal Union Nusu Fainali Azam Sports

Azam Vs Polisi Tanzania Azam yaichapa Polisi Tanzania na kutinga hatua ya Nusu Fainali

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji. Timu ya Azam FC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo uliopigwa Jumatano Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na Rodgers Kola dakika ya 24, Ismail Aziz Kader dakika ya 45 na Mudathir Yahya dakika ya 78 na sasa Azam FC watamenyana na Coastal Union ya Tanga iliyoitoa Kagera Sugar.

Timu nyingine iliyotinga Nusu Fainali ni Yanga ambayo imeitoa Geita Gold na itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho baina ya mabingwa watetezi, Simba na Pamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live