Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC wanasafiri jioni ya leo kuelekea nchini Misri tayari kabisa kuvaana na wenyeji timu ya FC Pyramids.
Msafara wa Azam FC, ambao umejumlisha wachezaji 25 umeshawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tayari kwa safari, kuelekea jijini Cairo, Misri.
Azam itacheza mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids utakaofanyika Uwanja wa June 30, Jumamosi hii saa 4.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya bila kufungana katika Uwanja wa Chamazi Jijini Dar es Salaam.