Matajiri wa Jiji Azam FC, wamelazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya FC Pyramids kutokea nchini Misri.
Mchezo huo wa hatua za awali kufuzu kwa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika ulio[pigwa katika dimba la Azam Complex, umeisha kwa sare ya 0-0.
Timu ya Pyramids FC ambayo wengi wanaipa nafasi kubeba Kombe hili kutokana na uwekezaji wake mkubwa uliofanya, imecheza kwa tahadhari kubwa kuhakikisha hawaruhusu goli ili wakapate urahisi katika mchezo wa marudiano.
Azam watasafiri kuwafuata FC Pyramids nchini Misri katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 23.
Inatazamiwa kuwa mechi ngumu kwa upande wa Azam FC ikizingatiwa namna ambavyo timu za Misri zinatumia vyema viwanja vyao vya nyumbani.
Sare ya aina yoyote ya kufungana itawapa Azam FC faida ya kusonga mbele kwa hatua zinazofuata.