Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam ni timu bora kuliko Simba - Mchambuzi

Azam FC Dubeeeeeee Azam ni timu bora kuliko Simba - Mchambuzi

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitria EA Radio, Ibra Kasuga amesema kuwa kwa sasa Kikosi cha Azam FC ni bora zaidi kuliko Simba Sc na kwamba Wakanda Ngano hao ndiyo timu pekee wanayoweza kuwapa changamoto Yanga.

Kasuga amesema hayo baada ya Azam kupata matokeo mazuri katika mechi za hivi karibuni na kuifanya iongoze ligi japo Simba na Yanga wana michezo kadhaa ya viporo.

"On paper kwenye situation ya hivi sasa Azam wanaonekana kuwa na timu ya uhakika zaidi kuliko Simba kwenye makaratasi. Kwa upande wa Simba kunaonekana kwanza hakuna utulivu kuanzia nje mpaka ndani.

"Simba ukiangalia mpaka hivi sasa kuna baadhi ya maeneo unaona kabisa wanatafutana wenyewe wanajiona kabisa ubora hakuna.

"Lakini ukija Azam kwenye msimu huu wa mashindano kuna maeneo yanaonekana kwamba tayari wameshajipata, eneo kubwa sasa hivi ambalo linaimbwa kuhusiana na Azam watu wanaimba kwenye upana wa kikosi.

"Kwa hiyo ukiangalia Azam uwanjani wana wachezaji ambao wana-perform, na kuna wachezaji ambao wako benchi lakini wakipata nafasi ya kuingia nao pia kuna kitu ambacho wanaenda kutoa kwa quality ile ile," amesema Ibra Kasuga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live