Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam na dakika 180 Bara

Dabo Kocha Azam Azam na dakika 180 Bara

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo, amesema mechi mbili zilizosalia za Ligi Kuu Tanzania Bara ni 'muhimu mno' wachezaji wake kuonyesha ukomavu na kutumia vizuri kila nafasi itakayopatikana ili kujihakikishia wanavuna pointi sita.

Azam imebakiza mechi dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam itamaliza msimu ugenini kwa kuwafuata Geita Gold FC, mchezo utakaochezwa Mei 28, mwaka huu.

Dabo alisema ana kazi ya kuendelea kutengeneza mazingira mazuri ya wachezaji wake kuhakikisha hawapotezi nafasi ili kuondoka na ushindi wa idadi kubwa ya mabao na hatimaye kufikia malengo ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu ujao.

Kocha huyo alisema Alisema mechi mbili ni muhimu kushinda na wachezaji wanatakiwa kuwa wakomavu na kutengeneza utulivu wanapokuwa na hata wasipokuwa na mpira ili kufikia malengo yao.

“Sio rahisi kushinda mechi, nimeongea na wachezaji wangu wanatakiwa wawe watulivu katika kila mchezo na kutumia vizuri nafasi zinazopatikana, ni muhimu kupata pointi tatu lakini kwa sasa kushinda idadi kubwa ya mabao ili tufikie malengo yetu,” alisema Dabo.

Kocha huyo aliongeza wanahitaji umakini zaidi ili kuhakikisha hawapotezi alama hata moja kwa sababu wanajua wako katika vita ya kuwania nafasi ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live