Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam kuwavaa Wasomali leo, mechi zote Dar

Zaka Zakaziii.jpeg Zakaria Thabiti 'Zaka Zakazi', Ofisa Habari wa Azam FC

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji, Timu ya Azam FC imethibitisha kupokea taarifa kupitia Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) juu ya kutoruhusu Mashabiki katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Horseed FC ya Somalia.

Azam FC itawakaribisha Horseed katika mchezo huo wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa katika Uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabiti 'Zaka Zakazi', amesema hawana jinsi kutokana na taarifa hizo kutoka CAF, kwa sababu hali hiyo ni kutokana na changamoto za ugonjwa wa COVID-19 ambao dunia nzima inakabiliana nao kwa sasa.

Amesema kikubwa waliendelea kufanya maandalizi mazuri baada ya wachezaji wote walikuwapo kwenye majukumu ya timu za taifa kurejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Horseed FC.

"Wachezaji wote wamerejea kambini akiwamo nyota wa nje ambao walikuwa katika majukumu ya mataifa yao,

wanaendelea vizuri na tuko tayari kwa ajili ya kupambana kutafuta matokeo chanya dhidi ya Horseed SC," amesema Zaka.

Aidha mchezo wa Marudiano utapigwa katika Uwanja wa Uhuru hapa hapa Dar es Salaam Septemba 18, baada ya Timu hiyo kutoka Somalia kuomba kibali kwa CAF kutokana na hali ya usalama kutokua ya kuridhisha nchini Somalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live