Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam kuwakosa wanne dhidi ya Simba

Yousuf Dabo Azammm Azam kuwakosa wanne dhidi ya Simba

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Azam FC, Bruno Ferry amesema kikosi chake kitawakosa wachezaji wanne kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Simba, huku akiwatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwani kikosi chake kimejiandaa vizuri na kina kikosi kipana cha kupambana na kupata ushindi.

Azam itakuwa mgeni wa Simba kesho kuanzia saa 10 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo mastaa watakaokosekana ni Sospeter Bajana, Abdallah Heri ‘Sebo’, Malickou Ndoye na mshambuliaji Alassane Diao.

Ferry amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwakuwa wanakutana na timu bora yenye benchi la ufundi linaloongozwa na kocha mwenye wasifu mkubwa Afrika lakini na wao wamejiandaa vya kutosha, huku akitahadharisha na kutaka marefa wachezeshe kwa haki na atakayepata ushindi uwe ushindi sahihi.

“Ni mchezo muhimu tumejiandaa vizuri na tuko tayari kwa mchezo. Wapinzani wetu ni wazuri tunajua wana benchi zuri na wachezaji bora na tunafahamu ukiwa Simba una presha ya kushinda. Natumaini kesho mambo yatakwenda vizuri na mchezo utavutia,” amesema Ferry na kuongeza:

“Utakuwa mchezo wenye presha, lakini tunahitaji uamuzi sahihi kwa timu zote. Hatuhitaji kushinda ama kushinda kwa sababu ya uamuzi usio sahihi kwahiyo tunaomba marefa watende haki. Itakuwa ni mapambano na wachezaji wako tayari kupambana, tunafahamu ni mchezo wa presha lakini tumemudu kupunguza hiyo presha.

“Tumejiandaa vizuri kwa siku chache zilizopita na tutegemee wachezaji wapya kuonekana kesho, japo wanazoea taratibu mazingira mageni wanahitaji kuchukua muda, lakini kimwili na kisaikolojia wako tayari kwa mchezo na kuisaidia timu. Tunahitaji mashabiki wetu, tuna wachezaji wa daraja la juu na benchi la ufundi bora kwa hiyo tuko tayari.”

Nyota wa timu hiyo, Lusajo Mwaikenda amesema kikosi chao hakiangalii wapinzani wao wanafanya nini, lakini wanachozingatia kwa sasa ni kuzicheza mechi zinazowahusu kwa kushinda na kuhakikisha wanatimiza malengo waliyojiwekea.

“Timu yetu iko tayari kwa mpambano wa kesho. Wachezaji wana morali ya juu, wachezaji wa Azam ni wakubwa na wanatamani kucheza michezo mikubwa kama hii. Tunawaheshimu Simba kwa ubora wao, lakini hiyo hatufanyi tushindwe kupambania malengo ya timu yetu,” amesema Mwaikwenda, kisha akaongeza:

“Timu msimu huu tulikuwa na malengo yetu. Tutaingia na nguvu ileile tunayoingia kwenye michezo mingine. Simba ni timu kama nyingine na sisi tuko tayari kucheza sehemu yoyote na tunaamini kwa ‘mentality’ tutakayoingia nayo itatusaidia kupata ushindi. Naamini mwalimu wetu ameandaa mbinu na mpango mzuri wa mechi na ‘focus’ yetu yote itakuwa kupata alama tatu na hii itatusaidia kuona tunasimama wapi katika msimamo wa ligi,”

Hawana hofu Ofisa Habari Msaidizi wa Azam, Hashim Ibwe amesema kukosekana kwa wachezaji wanne katika mchezo wa kesho hakuwapi hofu kwa sababu wana kikosi kamili kinachoweza kupambana kwenye mchezo wowote na kushinda, huku akitambia usajili mpya walioufanya dirisha dogo ambao utaziba pengo na wako tayari kwa mchezo.

“Ni mchezo ambao tuliusubiri kwa muda mrefu na kusubiri siku ifike hatimaye siku imefika. Maandalizi kwetu ni mazuri, tuko tayari kwa hiyo mechi na tunayo sababu ya kushinda. Kama timu hatutaki kujua tuko na nani pale juu. Tunachotaka ni kushinda kila tunayekutana naye. Mchezo wa kesho ni miongoni mwa michezo ambayo tumeiwekea hesabu,” amesema Ibwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live