Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam kujichimbia Morocco kujiandaa Ligi ya Mabingwa

Popat Azam Nsz Azam kujichimbia Morocco kujiandaa Ligi ya Mabingwa

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC, imetangaza rasmi kuwa kambi yake ya kujiandaa na msimu ujao wa mashindano itakuwa nchini Morocco.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Thabit Zacharia maarufu Zaka Zakazi, jana alisema maandalizi yao ya msimu mpya (pre season) watafanyia nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la FA na safari hii Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo wataicheza kwa mara ya kwanza baada ya misimu 10.

Mara ya mwisho kwa Azam kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa ni msimu wa 2013/14 ilipotwaa Ubingwa wa Tanzania Bara.

Zaka Zakazi alisema wachezaji wa timu hiyo wa zamani na wapya wataanza kuripoti kuanzia Julai Mosi, na tarehe tano wataanza mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

"Tutafanya mazoezi Chamazi, hadi tarehe saba tutakwenda Zanzibar, tukifika tutafanya mazoezi siku hiyo hiyo hadi Julai 13, tutarudi Dar na tarehe 14 tutaondoka nchini Morocco kuweka kambi ndefu sasa na hiyo ndiyo 'pre season' yetu kwa msimu huu," alisema.

Alisema watakaa nchini Morocco hadi mwishoni mwa mwezi Julai ndipo watakaporejea, tayari kwa kufungua msimu mpya wa mashindano.

"Tutakuwa kule mpaka mwishoni mwa Julai tutarejea nchini kuja kumalizia maandalizi ya mwisho kabla ya kufungua msimu rasmi kwa mechi za Ngao ya Jamii, nadhani hapo kila kitu kitakuwa kiko tayari kwa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo tunaipa kipaumbele kwani ni muda mrefu hatujashiriki," alisema Zaka.

Azam imetangaza kufanya 'pre season' yake, siku chache baada ya Klabu za Simba na Yanga kutangaza zitakapokwenda kuweka kambi.

Simba imatangaza rasmi kuwa mwanzoni mwa Julai inatarajia kwenda kwenye Jiji la Ismailia nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya mwanzo wa msimu, huku Yanga ikisema safari hii itakwenda 'pre seasons' Ulaya, huku pia ikiwa na ziara nchini Kenya na Afrika Kusini ambako inatarajia kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live