Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam kufuta unyonge kwa Mbeya City

Azam Fc Mbeya.jfif Azam watakuwa wageni mbele ya Mbeya City

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya msimu uliopita Mbeya City kuinyanyasa Azam, leo wapinzani hao wanakutana tena kwa mara ya kwanza msimu huu ikiwa ni kuendeleza rekodi au kulipa kisasi na kuweka heshima.

Katika msimu uliopita, Mbeya City ilikusanya pointi nne ikianza sare ya 2-2 ugenini kisha ushindi wa 2-1 nyumbani kwa matajiri hao wa Chamazi, ambapo leo timu hizo zinakutana kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa zikiwa na sura mpya za makocha ambao kila mmoja anasaka heshima yake.

Azam msimu uliopita ilikuwa chini ya Abdihamid Moalin, ambapo kwa sasa inaongozwa na Mfaransa, Denis Lavagne huku City ikiachana na Mathias Lule na sasa ni Abdalah Mubiru wote raia wa Uganda.

Hadi sasa Azam wapo nafasi ya sita kwa pointi tano baada ya kushinda mechi moja na sare mbili, huku wapinzani wakiwa wamekusanya pointi nne na ikisha nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi.

Makocha hao wanakutana uso kwa uso wakikumbuka matokeo ya sare kwenye mechi zilizopita, ikiwa wenyeji walitoshana nguvu ya 1-1 na ndugu zao Prisons ilhali Azam ikibanana na Yanga 2-2.

Pia katika mchezo wa leo Jumanne, utawakutanisha vinara wa mabao kikosini, ambapo kwa City wanajivunia uwezo wa Sixtus Sabilo, huku wapinzani wakiwa na Tepsie Evance ambao kila mmoja ana mabao mawili.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz