Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam kuboronga, Fei Toto autaja uongozi, afunguka kwenda Simba

Fei Toto Msh Azam kuboronga, Fei Toto autaja uongozi, afunguka kwenda Simba

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Azam, Feisal Salum amezungumza baada ya timu yake kupata alama moja dhidi ya JKT Tanzania ikiwa ni siku chache baada ya kuondolewa kwenye michuano ya ya CAFCL katika hatua za awali kabisa.

Azam waliambulia sare ya bila kufungana na wajeda wa JKT Tanzania katika Dimba la Meja Jenerali Isamhuyo uliopo Mbweni Dar es Salaam mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

“Kuondolewa mapema kwenye CAFCL, sisi kama wachezaji haijakuta kitu. Viongozi wanajua tunatakiwa tushiriki kwa namna gani, tujipange vingi ili tuweze kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, kwa hiyo msimu huu tumetolewa lakini tutajipanga ili msimu ujao tufike hatua ya makundi.

“Fei Toto ni yuleyule kila siku ninasema, sijabadilika, mashabiki zangu waendelee kunisapoti, nitaipambania Azam FC na mambo mazuri yanakuja. Waache waongee kwa sababu huwezi kumzuia mtu kuongea, sisi kama Azam Fc tutaendelea kuipambania klabu yetu na si kingine. Ligi ndiyo imeanza na kila mchezaji anataka kuipambania timu.

“Kuhusu kuhamia Simba siwezi kuzungumzia hilo, wacha tuendelee na ligi kwanza, acha niipambanie timu yangu iliyopo mambo mengine yatakuja baadaye,” amesema Fei Toto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: