Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam inautaka ubingwa haswa

Azam Ubingwa 2022 Azam watakua na kibarua kigumu leo mbele ya KMC

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya mtoano na Al Akhdar ya Libya kwa jumla ya mabao 3-2, Azam FC sasa akili na mipingo yake yote ni kubeba ubingwa wa ndani.

Taarifa za kuthibitika zinasema uongozi wa timu hiyo juzi ulikaa na wachezaji wote na bechi la ufundi katika kikao kifupi ambacho ajenda yake ilikuwa ni namna gani matajiri hao wa Chamazi watabeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu huu.

Kocha Mfaransa Denis Lavagne alielezea jambo hilo huku akiweka wazi mikakati yake ili kufikia malengo ya kubeba ubingwa.

“Tumetolewa kimataifa, sasa tunarudi kwenye mashindano ya ndani, bado tunanafasi kubwa ya kufanya vizuri huku na kufikia malengo ambayo ni ubingwa,” alisema Lavagne na kuongeza;

“Sio kazi rahisi lakini inawezekana, kwa sasa ni kuwahimiza wachezaji kujitoa kwa asilimia zote kama walivyofanya kwenye mechi ya Akhdar, ile presha ndiyo naitaka.

Hatupaswi kudharau mechi, kwakuwa huku ndiko matumaini yetu yamebaki hivyo kama kila mmoja atatimiza majukumu yake basi malengo yetu yatatimia.”

Kiungo wa timu hiyo, Muivory Coast, Tape Edinho aliweka wazi kuwa; “Tulikuwa na malengo ya kufika mbali kimataifa lakini imeshindikana, sasa tumebaki na michuano ya ndani tu, hivyo tunahitajika kupambana zaidi ili kufanya vizuri huku.”

Azam kwa sasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na alama 11 ilzovuna baada ya kucheza mechi sita, kushinda tatu, sare mbili na kupoteza moja na mchezo leo itacheza na KMC uwanja wa Uhuru kuanzia saa 10:00 jioni.

Chanzo: Mwanaspoti