Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam imeupiga mwingi kwa Kipre JR

Kipre Jr Algier Azam imeupiga mwingi kwa Kipre JR

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Azam FC imefanya uamuzi mgumu wa kumuuza winga wake Kipre Junior kwenda MC Alger ya Algeria kwa dau linalokadiriwa kufikia Sh700 milioni.

Uamuzi wa kumuuza Kipre Junior umefanyika siku chache baada ya timu hiyo kumruhusu mshambuliaji Prince Dube aondoke baada ya mchezaji huyo kulipa kiasi kama hicho ambacho Azam imekipata kwa kumuuza Kipre.

Kwa maana hiyo katika dirisha hili la usajili, Azam FC imeingiza kiasi cha zaidi ya Sh1.4 bilioni kutokana na mauzo ya Kipre Junior na fedha ilizopata kutoka kwa Dube ambaye amevunja mkataba.

Kuna watu ni kama hawaelewi hivi uamuzi huo wa Azam FC na wamekuwa wakiukosoa kwa madai haikutakiwa kuruhusu wachezaji wake nyota kuondoka katika kipindi hiki ambacho inajiandaa na ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Dube ni mshambuliaji wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kufumania nyavu na Kipre Junior ameonyesha umahiri wa kupiga pasi za mwisho, pia hata kufunga mabao.

Kama ambavyo ilikuwa sahihi kwa Azam FC kumwachia Dube aondoke kwa kumpa sharti la kufuata vipengele vya mkataba kati yao ndivyo ambavyo ni jambo jema kwa timu hiyo kumwachia Kipre Junior ambaye alibakiza mwaka mmoja mkataba wake na Azam ufikie tamati.

Inasemekana Kipre Junior alianza kuonyesha dalili za kutokuwa na furaha Azam FC na aliuambia uongozi wa timu hiyo kupokea ofa ambazo zingefika mezani na ukishindwa kufanya hilo usijisumbue kumwongezea mkataba mpya kwani atamalizia uliopo ili aondoke bure hapo baadaye.

Kwa wasomi wa Cuba hiyo sio ishara nzuri na inakuonyesha ukibaki na mchezaji husika unakuwa umejitengenezea mazingira na uwezekano wa kujimaliza wewe mwenyewe kwani anaweza kushiriki kukuhujumu siku moja ukajikuta unapata matokeo mabaya zaidi.

Kwa vile mkataba wake ulibaki mwaka mmoja, uamuzi wa kumuuza ndio ulikuwa sahihi maana wamepata fedha nyingi ambazo zinaweza kuwapa nguvu za kunasa vifaa vya maana kwenye usajili wao.

Chanzo: Mwanaspoti