Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam ifanye jambo kwa kipa Mo’ Mustafa

Mohamed Mustafa D Azam ifanye jambo kwa kipa Mo’ Mustafa

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu wa 2022/23 na mwanzoni mwa msimu uliopita wa 2023/24 havikuwa vipindi vizuri kwa makipa wa Azam FC ambao walikuwa wakifanya makosa ya mara kwa mara yaliyokuwa yakiigharimu timu hiyo.

Ilionekana kama usajili wa kipa aliyefanya vizuri kwenye fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2021, Ali Ahamada angetibu shida yao langoni lakini akawa na udhaifu wa kuruhusu mabao ya kizembe jambo lililoichosha timu hiyo na kuamua kumsajili Abdulai Iddrisu kutoka Ghana.

Alionekana kama angeweza pia kutibu tatizo ambalo timu hiyo ilikuwa inataka kulitatua lakini naye akaingia katika nuksi ileile iliyomtesa Ahamada.

Nyakati fulani, Kocha Youssouf Dabo alijaribu kutaka kumwamini bwana mdogo Zuberi Foba lakini ndani ya muda mfupi imani yake haikuzaa matunda.

Hata hivyo, subira yavuta heri na baada ya kuhangaika na makipa hao, ikatua Sudan ikamchukua kwa mkopo kipa wa Al Merrikh, Mohamed Mustafa.

Kipa hasa ambaye tangu alipotua katika kikosi chao, Azam haijawahi kujuta kuwa naye kutokana na kiwango bora ambacho amekuwa akikionyesha ndani ya timu hiyo aliyojiunga nayo wakati wa dirisha dogo la usajili.

Kwanza ana kimo stahiki kwa nafasi yake ambacho ni kirefu, ni mzuri wa kuokoa hatari za ana kwa ana na mipira ya krosi lakini pia ni kipa wa kisasa kwa maana ana uwezo mkubwa wa kuchezea mpira kwa miguu.

Pia ni mtulivu awapo golini na hesabu zake ni sahihi na juzi kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania, alionyesha uwezo mwingine wa kuokoa mikwaju ya penalti.

Nadhani Azam inapaswa kupambana kuhakikisha jamaa anabaki jumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live