Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam hesabu kali nusu fainali Mapinduzi

Azam FC Mapinduzi Cup Azam hesabu kali nusu fainali Mapinduzi

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Azam FC kimetumia saa moja kujinoa tayari kwaajili ya mchezo wa pili wa Mapinduzi dhidi ya Jamhuri mchezo utakaoamua nani atinge hatua ya nusu fainali kwenye kundi lao.

Azam FC ipo kundi A ambalo linaongozwa na Malindi yenye pointi nne na Jamhuri inapointi moja huku Azam FC pia ikiambulia pointi moja.

leo timu hizo ndio zitaamua Malindi aende nusu fainali au mmoja kati yao atinge hatua ya hiyo wakiitaji kushinda mabao zaidi ya matatu.

Kocha Kali Ongala anasema kikosi chake kipo kamili tayari kwaajili ya mchezo huo wa kesho lengo lao ni kuhakikisha wanapata usindi na kutinga hatua inayofuata.

“Hatuna majeruhi kikosi kipo tayari kwaajili ya kupambania nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali tunahitaji ushindi wa kuanzia mabao matatu hilo linawezekana,” alisema na kuongeza;

“Tunawaheshimu wapinzani wetu na wao wanaisaka nafasi ambayo na sisi tunaipambania dakika 90 zitaamua nani bora zaidi ya mwingine.”

Chanzo: Mwanaspoti