Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam hawana shaka na Mbombo, wampa muda

Mbombo Mshambuliaji wa Azam FC, Idriss Mbombo

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Azam FC Vivier Bahati amesema kuwa wana imani kubwa na mshambuliaji wa timu hiyo Idris Mbombo licha ya wengi kumkosoa.

Kauli ya Bahati inakuja baada ya Mbombo kufunga mabao mawili na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, dhidi ya JKU kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex.

“Ni mchezaji mzuri anayejua kufunga na mwenye matumizi mazuri ya akili hivyo itamchukua muda kutokana na ugeni wake lakini kadri anavyofunga ndivyo anavyozidi kurejesha kujiamini zaidi,” amesema.

Bahati alisema kuwa changamoto anayopitia nyota huyo ni kutokana na kufananishwa na mfungaji bora wa timu hiyo msimu uliopita Prince Dube ambaye amekuwa akiandamwa na majeraha tangu Mei 26, mwaka huu.

“Kila mchezaji aliyeko Azam ana kiwango kikubwa kwa kuwa tulizingatia mambo mengi kwenye usajili msimu huu ili kupata wachezaji watakaotimiza kile tunachokitaka,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live