Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam: Tupo seriuos, tutampa Mzize mshahara mnono

Ukweli Kuhusu Mzize Kutakiwa Na Azam FC.jpeg Clement Mzize.

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam imesema kuwa imetupa ofa kwa Klabu ya Yanga wakitaka kunasa saini ya mshambuliaji kinda, Clement Mzize ambaye amekuwa na kiwango bora tangu amesajiliwa na yanga.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Azam, Hasheem Ibwe wakati akihojiwa kuhusu dili hilo huku Yanga nao wakidaiwa kuwa wameshamalizana naye baada ya kumuongezea mkataba kinda huyo kufuatia kunyatiwa na vilabu vingi ndani ya Tanzania na hata Ulaya.

Itakumbukwa kuwa, kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam uliopigwa mwezi Aprili 2024, licha ya Yanga kupoteza kwa bao 2-1, Mzize ndiye aliwatungua Azam dakika za mwanzo tu za mchezo huo.

“Jumamosi sisi hatuna upande sisi tunaenda kumuangalia mchezaji wetu tu ikimpendeza mungu.

"Ni kweli kuwa tumetuma ofa ya Clement Mzize kwa Klabu ya Yanga tunasubiri tuone kama tutajibiwa lakini ubaoni imewekwa pesa ya kutosha, mshahara wa kutosha na maslahi yote ambayo anastahili mchezaji mkubwa kama Mzize.

"Sisi hatutekenyi na tulishaacha masihara zamani sana tuko siriazi sasa hivi, huu uwanja msimu ujao kutoka giants hao kuna wachezaji mtawaona kama wakikubali kutupa.

"Hizi timu mbili za kariakoo Simba na Yanga kuna wachezaji wanne sisi tutakuwa nao msimu ujao wapo wazawa pia wapo wageni na baada ya ofa hii ya kwanza wiki inayoanza Jumatatu itatumwa ofa nyingine na kuna mwingine ni special sana zaidi ya wengine," amesema Hasheem Ibwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live