Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam Singida Big Stars zasaka historia Mapinduzi Cup

Azam Mapinduzi Semi Azam Singida Big Stars zasaka historia Mapinduzi Cup

Sun, 8 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matumaini ya Singida Big Stars kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mara ya kwanza yameshikiliwa na mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam utakaochezwa leo usiku katika Uwanja wa Amaan.

Tangu mashindano hayo yaanzishwe, Singida Big Stars haijatwaa ubingwa ambayo huandaliwa maalum ukwa ajili ya kusherehekea Mapinduzi ya Zanzibar.

Ni tofauti na Azam FC ambayo mwaka huu inasaka ubingwa wa sita ambapo hadi sasa inaongoza kwa kutwaa mara tano.

Timu hizo zitakutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza baada ya kuongoza makundi ambapo Azam FC iliongoza kundi A baada ya kukusanya pointi nne katika mechi mbili ikianza na sare ya bao 1-1 na Malindi na kisha kuichapa mabao 3-0 Jamhuri.

Singida Big Stars ilimaliza ikiwa kinara wa kundi B ikianza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM kisha sare ya bao 1-1 na Yanga

Kocha wa Azam FC, Kally Ongala alisema ubora wa vikosi ndio utaamua mchezo, huku akidai kuwa wamefanya maandalizi mazuri kuhakikisha wanatwaa taji hilo baada ya msimu uliopita kufungwa na Simba kwenye fainali.

“Hatutarajii kurudia makosa tumekuja na kikosi chetu chote, lengo ni kuhakikisha tunafanya vizuri. Tunawaheshimu wapinzani, tunatarajia mchezo mzuri na wa ushindani,” alisema.

“SBS wana timu nzuri na sisi pia ni bora, dakika 90 zitaamua nani ana uwezo mzuri zaidi ya mwingine.”

Hans Van Pluijm, kocha wa Singida Big Stars alifurahi timu yake kufika nusu fainali kwenye mashindano ambayo ni msimu wao wa kwanza kushiriki.

“Ni hatua kubwa sana tuliyofikia na tuna imani kubwa ya kufanya vizuri zaidi kwenye hatua hii na hatimaye kutinga hatua ya fainali na kutwaa taji la Mapinduzi, historia ambayo itaandikwa na kikosi changu hiki ambacho kimefanya makubwa,” alisema.

“Natarajia mchezo mzuri na wa ushindani, wachezaji wangu wote wapo kwenye ari nzuri na wana morali baada ya kutinga hatua ya nusu fainali wameniahidi kuwa wanataka kuingia fainali na kutwaa taji.” Mchezo mwingine wa nusu fainali utakuwa kesho kati ya Mlandege na Namungo FC utakaochezwa muda uleule.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live