Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam Media yazijaza mamilioni timu Ligi Kuu Bara

Bonus Pic Data Azam Media yazijaza mamilioni timu Ligi Kuu Bara

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Azam Media imetoa Sh 225.6 Bilioni kwenye udhamini wa haki ya matangazo ya televisheni kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Udhamini huo wa miaka 10 kuanzia msimu wa 2021/2022 kwa mujibu wa Tido Mhando Mtendaji mkuu wa Azam Media.

Alisema katika pesa hiyo, asilimia 67 ya pesa itakuwa malipo ya kila msimu kwa klabu moja kwa moja za timu za Ligi Kuu.

"Msimu wa 2021/2022, pesa ya udhamini itakuwa Sh12 bilioni, klabu zitapata Sh8 bilioni na sehemu zitakazosalia zitasaidia maendeleo ya soka, TFF na Bodi," alisema Tido na kuongeza.

"Pesa hiyo itakuwa ikiongezeka kila msimu, ambapo msimu wa 2022/2023 udhamini utakuwa 13.2 Bilioni na timu zitapata Sh 8.8 bilioni.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz