Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam: Mayele wa kawaida sana!

Mayele Na Mashabiki Yanga Mayele na mashabiki

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wala hawatishwi na Kikosi cha Yanga wala mshambuliaji wao wanayemuona tishio, Fiston Mayele, ambaye kwao wanamuona ni mchezaji wa kawaida tu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabity Zakaria ‘Zaka Zakazi’ na kuongeza kuwa, siyo Mayele tu, bali hata mchezo wenyewe dhidi ya Yanga kwao wanauona ni wa kawaida na wanakwenda kupata alama tatu.

Yanga watacheza na Azam FC, Aprili 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo wa duru ya kwanza uliochezwa kwa Mkapa, Azam walifungwa 2-0. Akimzungumzia Mayele na mchezo wenyewe, Zaka alisema: “Sisi hatumuogopi Fiston Mayele, kwa kuwa tulikutana na wachezaji wakubwa zaidi yake kama Ramadan Sobhi wa Pyramids lakini hakufurukuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live