Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam: Leo tunafuta uteja kwa Yanga

Azam Fc 221 1140x640.png Azam: Leo tunafuta uteja kwa Yanga

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Azam, Bruno Ferry amesema historia haina nafasi katika mchezo wa leo kati ya timu yao na Yanga Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Oktoba 22, 2023, Ferry amesema wanaiheshimu Yanga kuelekea katika mchezo huo na wataenda kuleta mshangao.

“Mchezo wetu wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ulikuwa ni mchezo wa maadalizi ya Ligi Kuu, hivyo huwezi kuwa sawa na huu, kwani sasa tupo katika ari nzuri zaidi kuliko mwanzo,” amesema kocha huyo.

Kwa upande mwingine Ferry ameahidi kuonesha mchezo wa kiungwana wenye ufundi wa hali ya juu.

“Utaenda kuwa mchezo maalumu ila tutajitahidi kadri tuwezavyo kuonesha mchezo mzuri na wenye ushindani,” amesema Ferry.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: