Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam, KMC  moto

3cc56b473d71ec8b37cf2a567dddb694 Azam, KMC moto

Wed, 23 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

LIGI Kuu Bara, msimu huu ukiwa ni mzunguko wa tatu mambo yamegeuka kwa vigogo na sasa timu za KMC na Dodoma jiji zinaonekana kuwa moto.

KMC iliyopata shida zaidi msimu uliopita imeanza kwa kasi tofauti na matarajio ya wengi na ndio kinara wa ligi hiyo ikiongoza kwa uwiano mzuri wa mabao baada ya kufikisha pointi tisa.

Aidha, Azam FC nao wamebadilika kwa kasi tofauti na walivyochukuliwa awali, wanafanya vizuri baada ya kucheza michezo mitatu na kushinda yote wakishika nafasi ya pili kwa pointi tisa wakiwa na mabao ya kufunga manne na hawajaruhusu bao kwenye nyavu zao.

Upinzani umekuwa mkali kwa Simba ambao ndio mabingwa watetezi mpaka sasa licha ya kurudi kwa kasi mchezo uliopita dhidi ya Biashara United, tayari wana sare moja waliyopata kwa Mtibwa Sugar na wanashika nafasi ya tatu kwa pointi saba wakiwa wamefunga mabao saba na kuruhusu mawili.

Ubora wa kikosi hicho msimu uliopita na maboresho ya kikosi chao msimu huu ilitarajiwa kuona Simba iliyo kali zaidi. Lakini ni kama ileile ikikabiliwa na upinzani katika mechi hizo za awali.

Pia, Yanga pamoja na usajili wao mkubwa msimu huu wanakabiliwa na upinzani mkali kwani wana sare moja waliyoipata nyumbani dhidi ya Prisons wakiwa wanashika nafasi ya tano kwa pointi saba wakifunga mabao matatu na kuruhusu moja.

Kingine Yanga inahangaika katika safu ya ushambuliaji haijaelewana kitendo kinachowapa wakati mgumu wa kufunga.

Simba na Yanga namna zilivyotajwa katika usajili wao pengine ilitarajiwa waongoze ligi na kufunga mabao mengi lakini mambo bado pengine michezo ijayo.

Timu kama Dodoma Jiji, Ihefu zilizopanda msimu huu zimeonesha mwanga kwa kuanza vizuri mechi zao zilizopita. Mtibwa msimu uliopita haikuwa vizuri ila inakuja taratibu huenda ikabadilika.

Biashara, Prisons, Polisi Tanzania, Ruvu Shooting, JKT Tanzania zinacheza katika nafasi zilizozoea za katikati hali sio shwari kwa Coastal Union, Kagera Sugar na Namungo bado sio wale wa msimu uliopita kwani hawajaonesha makali yao vile ipasavyo.

Mwadui na Mbeya City zinateseka tangu msimu uliopita hazikuwa bora na bado zinaendelea kuhangaika. Gwambina iliyopanda Ligi Kuu pia haijakaa vizuri huenda zote hizo zikabadilika baadaye kwa vile kuna michezo mingi mbele.

Chanzo: habarileo.co.tz