Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam Fc wanakamia Simba na Yanga?

Azam FC008 Azam Fc wanakamia Simba na Yanga?

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kauli zingine si za kimichezo, hivi unaanzaje kusema Azam FC wanaikamia Simba na Yanga?

Simba na Yanga ndiyo timu kubwa hapa nchini, Azam FC ndiyo timu inayotoa changamoto kwa hivi vilabu, mara kadhaa wamekuwa wakionesha kiwango bomba sana dhidi ya hizi klabu mbili, lakini inatokea watu wanasema Azam FC wanakamia.

Ifike mahala tutambue kuna utofauti mkubwa sana kati ya kukamia na morali ya mchezaji kwenye mechi husika. Wakiwa wanacheza na Wydad, Al Ahly, Simba wanakuwa kama Real Madrid, lakini kuna muda Simba wakikutana na Mbeya City, Coastal union, Mtibwa Sugar wanapata matokeo kwa tabu sana.

Kwa hiyo mjue kutofautisha mechi kubwa mchezaji hawezi kuingia lele mama. Ni Lazima akajitoe kwa nguvu zake zote na hadi za ziada. Hivyo Azam FC hawakamii bali wanajituma sana hasa wanapokutana na timu ambayo kwao ndiyo washindani wa kweli.

Ni kama Simba tu yupo radhi apoteze mchezo na Ihefu lakini siyo kupoteza dhidi ya Yanga. Mechi za Yanga na Simba haziitwi kukamiana zinaitwa Derby ilikuwa ya moto.

Lakini wakifanya hivyo Azam FC wanakamia, hii nchi, mtu anapokutana na mpinzani wake lazima atajitoa kivyovyote tu, lakini anapokutana na mpinzani wake wa kawaida anacheza mechi tu akini siyo kwa kiwango kile cha mpinzani wake wa kweli.

Ipo siku mtakuja kuiheshimu Azam FC, mpira ni mchakato unaochukua muda mrefu kama Simba na Yanga zinavyojitafuta Kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: