By OLIPA ASSAWACHEZAJI wa Azam FC hawataki kubweteka baada ya kushinda mechi sita zilizowafanya wang'ang'anie katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwani wameapa kupambana kwa kuwa kila mechi kwao wameamu kuiona kama fainali.
Kipa wa timu hiyo, David Kisu ameliambia Mwanaspoti, leo Jumanne ya Oktoba 20, 2020 kwamba licha ya kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi wanachukulia kama changamoto ya kulinda nafasi hiyo, hivyo kila mechi watapambana vilivyo ili washinde.
"Tunajua kwamba ligi ni ngumu, inahitaji kila mechi kujituma na kucheza kama fainali, hilo ndilo litafanya tufikie malengo yetu ya msimu huu kwa sababu na sisi tunatamani kuvaa medali ya ubingwa," amesema Kisu.