Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yazitaka pointi 15 za Novemba

Azam FC VV Kikosi cha Azam FC

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Azam FC umedhamiria kupata pointi zote 15 kwenye michezo yake mitano ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kucheza mwezi huu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi.

Michezo mitano Azam ni dhidi ya Dodoma jiji FC uwanja wa Azam Complex, Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting, Namungo FC na dhidi ya Coastal Union.

Kwa sasa Azam ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 17 katika michezo tisa mbayo wamecheza hadi sasa. Endapo watafanikiwa kukusanya pointi hizo 15 watafikisha alama 33.

Akizungumza na gazeti hili, Kocha Mkuu wa Azam, Kalimangonga Ongala alisema malengo yao ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika kila mechi ili kufikia kile kinachotarajiwa.

Alisema anajua hakuna mechi rahisi kwao na ushindani umekuwa mkubwa kwenye ligi hivyo yeye na wachezaji wake wanalazimika kupambana bila kuchoka ili kufikia kile ambacho wamekikusudia.

"Hakuna mechi rahisi tunatakiwa kujipanga vizuri katika mechi zote tutakazo cheza mwezi Novemba ili kutimiza lengo kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kutimiza wajibu wake naamini tukifanya hivyo uhakika wa ubingwa msimu huu ni mkubwa,” alisema Ongala.

Alisema anajua mapambano kati yao na watani zao ni makubwa lakini kitu cha msingi yeye anaangalia zaidi mechi zao kuhakikisha wanacheza vizuri na kupata ushindi mwisho wa msimu ndio atajua timu gani imekuwa bingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live