Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yawawekea ngumu Simba, Yanga

Kipreee.jpeg Kipre Jr.

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC, wamezishtukia klabu kongwe hapa nchini Yanga na Simba baada ya kuwapa masharti MC Alger ya Algeria kwa kuweka kipengele kigumu katika mkataba wa mauzo ya kiungo wao Kipre Junior kipengele hicho kikimtaka kiungo huyo ikiwa atataka kurejea kucheza Tanzania kuwataarifa waajiri wake hao yaani First Refusal.

Nyota huyo amekuwa akizungumzwa na Yanga na Simba ambazo zimeonesha nia ya kumuhitaji baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika misimu miwili aliyodumu ndani ya Azam FC, taarifa za kuaminika ni kuwa Kipre amekamilisha usajili na kujiunga na MC Alger na Azam FC watapata kiasi cha dola 200,000 na 220,000 baada ya kukamilika kwa dili hilo.

Imeelezwa kuwa Azam FC wamekubali kumuuza mchezaji huyo mwenye mkataba wa mwaka mmoja na Januari mwakani alikuwa anabakisha miezi sita ambayo ingewaweka kwenye hatari ya kumpoteza bure.

“Ni kweli hilo dili lipo mezani na mazungumzo yanaenda vizuri, viongozi wameamua kukubali ofa hiyo na kuweka kipengele, atahitaji kurejea Tanzania  kwanza awombe kabla hajachukuwa maamuzi ya kwenda kwenye klabu nyingine wakihofia nyota huyo kutua mmoja ya klabu kongwe hapa nchini,” chanzo chetu cha habari kimetuambia.

Spotileo ilimtafuta Ofisa habari wa Azam FC, Thabit Zakaria (Zaka zakazi), ambaye amesema hawajamuweka mchezaji huyo sokoni, wapo tayari kupokea ofa kwa klabu inayomuhitaji akiwemo nyota huyo.

Amesema wanaona taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa Kipre anatakiwa Algeria, hawajapokea ofa yoyote lakini wamefungua milango wazi kwa klabu inahitaji huduma ya nyota wake huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: