Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yatoa Ujumbe mzito kwa Mashabiki wake

Azam Shukran Mashabiki Azam FC yatoa Ujumbe mzito kwa Mashabiki wake

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu wa Soka 2023/24 ukiwa umetamatika Juni 2, Klabu ya Azam FC leo Juni 4 kupitia kurasa zake Rasmi kwa Klabu imetoa Ujumbe wa Shukrani kwa Mashabiki wao.

Ujumbe huo wa Matajiri hao wa Jiji unasomeka kama ifuatavyo;

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa mashabiki wetu na wapenzi wetu wote kwa kutuunga mkono toka mwanzo hadi mwisho tulipomaliza msimu wa 2023/24.

Hakika mmepambana sana kwa nguvu nje ya uwanja kila sehemu tulipokuwepo kwenye mapambano, licha ya uchache wenu.

Tunawaomba msituache bali muendelee kuwa nasi zaidi kwenye msimu ujao, ili tuweze kufikia mafanikio zaidi kwa pamoja kwani nyie mmekuwa watu muhimu sana katika mafanikio yetu.

Hatuna mengi ya kuwaambia, tukutane tukiwa na nguvu zaidi na imara zaidi kwenye mapambano yetu yajayo msimu ujao 2024/25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live