Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yatinga Robo Fainali Kombe la TFF

Azam Robo Finalll Azam FC yatinga Robo Fainali Kombe la TFF

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Azam FC wamefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jana Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo Feisal Salum dakika ya kwanza, Ayoub Lyanga dakika ya 28 na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 69.

Azam FC inakuwa timu ya sita kwenda Robó Fainali ya michuano hiyo baada ya Singida Black Stars, zamani Ihefu SC, Coastal Union, Namungo FC, Geita Gold na Tabora United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live