Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yashusha kifaa toka Mali

Beka Azam Mali Azam FC imefikia makubaliano ya kumnunua beki wa kimataifa wa Mali, Yoro Mamadou Diaby

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam FC imefikia makubaliano ya kumnunua beki wa kimataifa wa Mali, Yoro Mamadou Diaby, kutoka Kituo cha Soka cha Yeleen Olympique cha nchini humo.

Mlinzi huyo wa kati ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Stade Malien de Bamako iliyofika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, atajiunga rasmi na Azam FC kuanzia msimu ujao wa 2024/25.

Yoro amezichezea timu zote za vijana za taifa za Mali, kuanzia ile ya chini ya 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki CHAN, mwaka 2022 nchini Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live