Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yapania kuharibu rekodi ya Mgunda

Mgunda Neno Staa Azam FC yapania kuharibu rekodi ya Mgunda

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Azam FC, kupitia kwa Kaimu Ofisa Habari wake, Hashim Ibwe umewataka mashabiki wake kununua tiketi kwa wingi ili kwenda kucheki mastaa wao wanavyoenda kuharibu rekodi ya Kocha wa Simba, Juma Mgunda, leo.

Mgunda tangu ajiunge na Simba Septemba 8 ambapo hadi sasa ameiongoza timu hiyo kwenye michezo saba za mashindano yote, ameshinda sita na moja ametoa sare kati ya hizo za ligi kuu ni tatu ambazo ameshinda mbili na moja sare zilizobaki ni za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Azam FC ambayo inanolewa na Kally Ongala leo Alhamisi inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao utapigwa katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Mechi yao ya mwisho timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Ibwe alisema kwamba, wana uhakika wa kuvuna ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Simba kwani tayari wameshategua mitego yote ambayo Simba huku nyota wao, Prince Dube na Rogers Kola wakiwa tayari kuwapa furaha mashabiki wao.

“Naomba ushikilie maneno yangu kwamba leo ndiyo siku pekee ambayo tunaenda kusambaratisha rekodi ya Simba kwa kocha wao Mgunda, kwani tayari hali za wachezaji wetu wote ziko sawa hivyo tuna uhakika wa kujipatia ushindi wa mapema kabisa hapo kwa Mkapa.

“Nitumie fursa hii kuwaomba mashabiki zetu wote waje kwa wingi ili waweze kupata furaha ya moyo ambayo ilitaka kupotea baada ya kupoteza mchezo wetu wa mwisho dhidi ya KMC,” alisema Ibwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live