Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yaondoa jina la Dube kwenye orodha ya wachezaji wake

Prince Dube 1 Prince Dube.

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam imeliondoa jina la mshambuliaji wao raia wa Zimbabwe, Prince Mpumelelo Dube (27) kwenye system ya usajili wa TFF kwa wachezaji kama mchezaji ambaye hataitumikia klabu hiyo.

Prince Dube yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu zote za kimkataba ili kuachana na klabu ya Azam, ambapo klabu ya Azam ilikubali mchezaji huyo aondoke lakini alipestahiki zote za kimkataba zilizopo baina ya pande zote mbili.

Hii inakuja baada ya Dube kuandika barua kwa uongozi wa Klabu hiyo akiomba kuondoka huku viongozi hao wakimtaka alipe kiasi cha dola 300,000 kama thamani ya kuvunja mkataba.

hata hivyo, Dube amesharudisha nyumba na kila kitu alichopewa na Azam FC huku akifuta picha zake zote alizopiga akiwa na nembo ya Azam na kutangaza kuondoka ndani ya Klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: