Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yamuibua Manara

Semaji, Haji Manara Msemaji wa Yanga, Haji Sunday Manara

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers

Afisa Habari wa Yanga,Haji Manara amesema kuwa licha ya kutambua ubora wa Azam FC lakini anaamini kuwa kikosi cha Yanga kina uwezo mkubwa wa kuondoka na ushindi mbele ya Azam FC.

Yanga Oktoba 30, katika Uwanja wa Benjamini Mkapa watakuwa na kibarua cha kucheza na Azam FC huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa bao 1-0 walipocheza na timu hiyo katika mchezo wa mwisho wa ligi kukutana ambapo ilikuwa msimu uliopita.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Manara amesema kuwa kuelekea katika mchezo huo wanafahamu kuwa utakuwa ni mchezo mgumu kwao lakini anaamini kuwa ubora wa kikosi cha Yanga utaenda kukipa ushindi dhidi ya Azam FC.

“Tunatambua ubora wa Azam katika ligi kuu ni timu nzuri lakini hilo halitufanyi sisi tushindwe kupata matokeo mbele yao, Yanga kwa sasa tunatimu bora ya kucheza na timu yeyote na tukapata ushindi hivyo tunatarajia kupata ushindi mbele ya Azam FC,”amesema Manara.

Yanga kwa sasa ndiyo vinara wa ligi kuu wakiwa wanaongoza ligi hiyo kwa pointi tisa mara baada ya kushinda katika michezo yote mitatu waliyocheza.

Chanzo: globalpublishers