Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yamshusha Mamadou Samake kutoka CR Belouizdad

Mamadou Samake A0003 Azam FC yamshusha Mamadou Samake kutoka CR Belouizdad

Sat, 20 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam Fc imethibitisha kukamilisha usajiliwa kiungo mkabaji Mamadou Samake kwa mkataba wa miaka miwili akitokea kwa miamba ya soka nchini Algeria, CR Beloujzdad.

Samake (24) raia wa Mali anafunga rasmi usajili wa Wanalambalamba hao kwenye dirisha hili kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25 na anatarajia kujiungana kambi ya timu hiyo nchini Morocco muda wowote kuanzia sasa.

"#DoneDeal Tumeingia mkataba wa miaka miwili na kiungo mkabaji, Mamadou Samake, akitokea kwa miamba ya Algeria, CR Belouizdad.

"Samake, anafunga rasmi usajili wetu kwenye dirisha hili kwa ajili ya msimu mpya 2024/25.

"Kiungo huyo mahiri, 24, anatarajia kujiunga na kambi ya timu nchini Morocco muda wowote kuanzia sasa, tayari kujiandaa vilivyo na msimu. Welcome to Azam FC mwamba, Samake!" Imesema taarifa ya Azam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live