Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yamruhusu Prince Dube kuvunja mkata

Dube Kofia.jpeg Azam FC yamruhusu Prince Dube kuvunja mkata

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC imesema kuwa, ipo tayari kumuachia mshambuliaji wao wa Kimataifa raia wa Zimbabwe, Prince Dube kuondoka ndani ya klabu hiyo kama ambavyo mwenyewe ameomba.

Azam FC imeweka bayana kuwa haina kipingamizi chochote na imemruhusu Dube kuondoka lakini matakwa ya kuvunja mkataba huo yafuatwe.

Ikumbukwe kuwa mkataba mpya wa nyota huyo raia hiyo aliyosaini mwaka 2023 ulipaswa kufikia ukingoni Juni 2026.

Akifafanua hilo, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria 'Zakazakazi' amesema;

“Kama anadhani kwamba kuna klabu inamtaka basi ije mezani izungumze na Azam FC kwa masharti kwamba gharama yake ya kumnunua ni dola laki 3 na sharti la pili alilopewa ni kukaa klabuni mpaka mkataba wake utakapoisha.

“Kama moja ya masharti haya yatatekelezwa, basi Dube ana ridhaa ya klabu kuondoka. Dube hana shida yoyote, ni kijana wetu ambaye amekaa kwenye klabu kwa miaka yote tangu 2020. Mkataba ni suala la kisheria, yoyote atakayekiuka utamuadhibu.

“Azam FC kwa kuogopa kuadhibiwa na mkataba wenyewe unavyohitaji, inataka kuuheshimu mkataba na inamtaka mchezaji kuuheshimu mkataba kama unavyosema siyo kuomba kuondoka kwamba klabu imwachie tu kuomba kuondoka, atakuwa anakiuka mkataba.

“Kwa hiyo Azam FC haimzuii Dube kuondoka, iko tayari kushirikiana naye kutekeleza kilichopo kwenye mkataba, kitakapotekelzwa mchezaji yupo huru kwenda anakokutaka,” amesema Zakazakazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: