Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yajibu madai ya kuwa tawi la Simba

Zaka1 Azam FC yajibu madai ya kuwa tawi la Simba

Wed, 20 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC imekanusha vikali kauli za wadau wengi na mashabiki wa soka nchini kuwa ina mahusiano na klabu ya Simba hasa katika masuala ya ndani ya uwanja.

Hayo yameelezwa na Afisa Habari wake, Zakaria Thabit 'Zaka Zakazi' alipokuwa katika mahojiano na Kipenga Xtra ya East Africa Radio, ambapo amesema kuwa habari hizo hazina ukweli na ni ukosefu mkubwa wa heshima kwao.

Kumekuwepo na habari kwa mashabiki wengi wakiituhumu Azam FC kuwa inapendelea Simba kuliko Yanga na hata kudai kuwa katika mechi wanazokuta timu hizo, Azam imekuwa haioneshi ushindani mkali kwa Simba kama inavyoonesha kwa Yanga.

"Watu wanatukosea sana heshima, sisi si tawi la Simba na wala hatuna uhusiano wowote, wao wanaoongea hivyo watambue wanawakosea sana heshima wamiliki wa klabu ambao wamewekeza mabilioni ya pesa. Kama tungekuwa ni tawi lao basi tungewapa uwanja wetu", amesema Zaka Zakazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live