Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yaingia mafichoni rasmi

Azam Official Team Azam FC yaingia mafichoni rasmi

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Azam FC kimeingia kambini rasmi juzi kuanza maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), dhidi ya Simba utakaopigwa Mei 6, Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara.

Wakati timu hiyo ikirudi mazoezini baada ya mapumziko ya muda mfupi, kocha mkuu wa kikosi hicho, Kally Ongala alisema amefurahishwa na urejeo wa nyota hao huku akiweka wazi wako na morali zuri.

"Kila mmoja wetu yuko kwenye hali nzuri wakati tukijiandaa na mchezo huo mgumu na muhimu kwetu, hili ndilo kombe tunaloona tuna nafasi kubwa ya kulichukua hivyo lazima tujipange," alisema.

Kally aliongeza licha ya kutokuwa na mchezo wowote kabla ya kukutana na Simba ila sio sababu ya kuwatoa kwenye mstari na kuwafanya kushindwa kutimiza malengo yao kwani kimwili na kiakili wako vizuri.

Azam inakutana na Simba huku mchezo wao wa mwisho kucheza ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting na kuweza kushinda mabao 3-1, katika mechi iliyopigwa Aprili 22, Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Azam iliweza kuiondosha Mtibwa Sugar kwa kuifunga mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali ya (ASFC), huku kwa upande wa Simba ikitinga hatua hiyo kibabe kufuatia ushindi mnono wa 5-1 dhidi ya Ihefu.

Chanzo: Mwanaspoti