Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yafafanua usajili wa Alassane Diao

Diao Oo.jpeg Azam FC yafafanua usajili wa Alassane Diao

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Azam FC umeeleza kuwa Mshambuliaji Msenegali, Alassane Diao waliyemsajili kutoka US Goree walimchukua akiwa huru na hakuwa na mkataba na klabu hiyo kama inavyoelezwa.

Uongozi wa Azam FC imeeleza hayo baada ya Goree kutoa taarifa kwa umma kuwa Diao ni mchezaji wao halali na amesajiliwa akiwa na mkataba na timu hiyo, hivyo wanajipanga kuchukua hatua za kisheria.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Azam FC kuwa kwanza wao hawana taarifa rasmi za malalamiko hayo zaidi ya kuona mitandaoni lakini wao wana nyaraka zote sahihi zinazoonesha mchezaji huyo alikuwa huru wakati wanamsajili.

“Kama kweli wana mkataba naye walete malalamiko rasmi kwetu, pili tulishawasiliana na kambi ya mchezaji na kuthibitisha juu ya kumalizika kwa mkataba wake. Isipokuwa mkanganyiko uliopo umetokana na kusogezwa mbele kwa msimu wa ligi ya Senegal.

“Kilichotokea ni ligi yao kusogezwa mbele na kufanya mkataba wa Diao kumalizika kabla ya ligi kuisha, wao walipaswa wamwombe mchezaji amalizie ligi wakati huo lakini wanasema ni mchezaji wao halali wakati kimsingi amemaliza mkataba,” amesema Zakaria.

Ligi Kuu ya Senegal maarufu Ligue 1 inayoshirikisha timu 14 mpaka sasa imecheza mechi 23 zikiwa zimesalia mechi tatu kabla ya kufungwa rasmi kwa pazia la ligi hiyo.

Chanzo: Dar24