Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yafafanua kuwabakisha Simba SC Kwa Mkapa

Hashim Ibwe Azam FC yafafanua kuwabakisha Simba SC Kwa Mkapa

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Azam FC umetoa ufafanuzi wa kuhamisha mchezo wao dhidi ya Simba SC kutoka Uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuupeleka Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mapema leo Jumatatu (Oktoba 24) Bodi ya Ligi ‘TPLB’ ilitoa ratiba ya michezo ya Mzunguuko wa tisa wa Ligi Kuu na kuthibitisha kuwa, mchezo wa Azam FC dhidi ya Simba SC utachezwa Uwanja wa Mkapa.

Afisa Habari wa Muda wa Azam FC Hashim Ibwe amesema, maamuzi ya kuhamisha mchezo huo kutoka Azam Complex na kuupeleka Uwanja wa Mkapa, ni maamuzi yaliyofikiwa na Uongozi wa klabu, na wala hawajashinikizwa na yoyote kufanya hivyo.

Ibwe amesema Uongozi wa Azam FC imechukua uamuzi huo kwa lengo la kutoa nafasi kwa Mashabiki wengi kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa, tofauti na Uwanja wa Azam Complex ambao unachukua idadi ndogo ya Mashabiki.

“Haya ni maamuzi ya Uongozi wa Azam FC, hatujashinikizwa na yoyote kuhamisha mchezo wetu kutoka Uwanjani kwetu hadi Uwanja wa Mkapa, tunaamini maamuzi haya yatawanushaisha Mashabiki wengi kufika Uwanjani na kuzishuhudia timu zote zikicheza soka la ushindani,”

“Tumaanini wapinzani wetu wana mashabiki wengi ambao wanahitaji kuuona mchezo huu, hali kadhalika hata upande wa Azam FC mashabiki wetu nao wanahitaji kuja kwa wingi kuutazama mchezo wetu na Simba SC, tumeona Uwanja wa Mkapa ni mahala sahihi kufika kwa wingi tofauti na Uwanja wa Azam Complex Chamazi.”

“Mchezo utapigwa majira ya saa moja usiku, hivyo tunawasisitiza Mashabiki wajitokeze kuzishuhudia timu zao zikicheza katika Uwanja wa Mkapa siku ya Alhamis.” amesema Ibwe

Azam FC inaekelea katika mchezo huo ikiwa chini ya uangalizi wa Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala na msaidizi wake, Agrey Moris, baada ya kumfukuza Kocha Denis Lavagne.

Jana Jumapili (Oktoba 23) saa 10 alasiri Kikosi cha Azam FC kilianza Programu yao ya mazoezi kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC.

Kwa upande wa Simba SC wanakwenda kwenye mchezo dhidi ya Azam FC, huku wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Watani zao wa Jadi Young Africans jana Jumapili (Oktoba 23).

Chanzo: Dar24