Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yaanza na sare Ligi Kuu, yaangusha alama mbele ya JKT

Azam Jkt Mszzz Azam FC yaanza na sare Ligi Kuu

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Azam chini ya Kocha Youssouf Dabo kimeanza kwa sare ya bila kufungana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Mechi ya kwanza ya Azam imepigwa leo dhidi ya JKT Tanzania katika Dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam huku zikishuhudiwa dakika 90 zikimalizika bila timu yoyote kufumania nyavu za mwenzake.

Azam ambao walimaliza msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya pili na kuwafanya kwenda kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambako nako waliondolewa na APR ya Rwanda mwishoni mwa wiki iliyopita.

Full time: JKT 0-0 AZAM FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: