Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yaanza na Moto Ligi ya Vijana, Yanga....!

IMG 7154 Azam FC yaanza na Moto Ligi ya Vijana, Yanga....!

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Azam FC imeanza vyema Ligi ya Vijana U20 baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Azam Academy yamefungwa na Ashraf Kibeku moja, Mahmoud Haji matatu na Clement Richard moja pia.

Mchezo mwingine wa leo wa Ligi Vijana U20, Yanga imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na KMC Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya KMC yote yamefungwa na Maulid Tamila, wakati ya Yanga yamefungwa na Karim Shija na Henry Francis.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live