Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yaanika jeshi lake 2021/2022

Azaaam Fccc Kikosi cha Azam FC 2021/2022

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji Azam FC, hii leo wameanika kikosi kamili kitakachokwenda kupambania kombe la Ligi kuu Tanzania Bara na lile kombe la Shirikisho barani Afrika kwa msimu wa 2021/2022.

Kikosi hiko cha maangamizi cha Azam FC kina wachezaji 29, chini ya Kocha Mkuu George Lwandamina.

Azam kwa muda mrefu sasa hawajashinda ubingwa wa Ligi kuu licha ya kuonekana ni timu yenye uwezo wa kushindana na vigogo Simba na Yanga kuanzia Uwanjani mpaka Uwekezaji.

Vile vile msimu mpya wa 2021/2022 Azam FC itakuwa na kibarua kizito cha kuiwakilisha nchi katika Mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kwa aina ya usajili na wachezaji waliowaongeza katika kikosi chao, ni dhahiri kuwa Azam FC italeta ushindani mkubwa msimu ujao.

Pengine labda tusubiri kuona matunda ya ile kambi ya maandalizi ambayo walikwenda kuiweka kule Ndola nchini Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live