Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC wazidi kuwekeza kwenye teknolojia

Azam FC008 Azam FC wazidi kuwekeza kwenye teknolojia

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam nao wameshusha machine ya kisasa iitwayo "Ball launcher" hii ni club ya pili Sasa kumiliki kifaa hicho na club ya kwanza ikiwa ni Young African Sports Club.

Hii machine ina balaa sana kwenye kuimarisha viwango vya wachezaji kwenye uwanja wa mazoezi.

Ball Launcher inaweza kuachia Cross aina zote ikiwemo in-swing na out-swing, hivyo inawasaidia walinzi wako kujifunza njia sahihi ya kuzuia mipira ya cross na Deadballs.

Pia, Football Launcher inaweza kuachia pasi mpenyezo kwenye eneo lolote la uwanja tena kwa kasi ya juu sana, hivyo inawasaidia washambuliaji wako kufanya mikimbio sahihi kwenye box la wapinzani na kumalizia nafasi.

Pia Ball Launcher inasaidi kuimarisha uwezo wa golikipa kwani kifaa hicho kinaweza kuachia kila aina ya shuti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live