Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC watamu bwana, waitandika Pamba goli 2

Azam Leo Azam waichapa Pamba mechi ya Kirafiki

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Azam kimeanza maandalizi yake jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United utakaopigwa Jumatano Februari 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma.

Katika maandalizi hayo Azam leo imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Timu hizo zimekutana baada ya kufanya vizuri kwenye michezo yao ya kombe la Shirikisho la Azam na kutinga hatua ya robo fainali ambapo Azam iliing'oa Baga Friends huku Pamba ikiondosha Dodoma Jiji.

Wachezaji wa timu ya Pamba wakiwa katika Picha ya pamoja na mchezaji wa Azam, Prince Dube baada ya kumkabidhi keki ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Mabao ya Azam yalifungwa katika kipindi cha pili mnamo dakika ya 59 na Rogers Kola huku la pili likifungwa dakika ya 64 kupitia kwa Prince Dube baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa suluhu (0-0).

Katika mchezo huo Azam ilianza kipindi cha kwanza kwa kuchezesha kikosi cha akiba kabla ya kuingiza kikosi cha kwanza kwenye dakika 45 za kipindi cha pili kikosi hicho kikiongozwa na Tepsi Evance, Prince Dube, Ibrahim Ajibu, Bruce Kangwa, Rogers Kola na Yahya Zayd.

Kocha wa Azam, Abdi Hamid Moallin amesema kikosi chake kimecheza vizuri na kinampa matumaini ya kufanya vizuri mchezo ujao wa ligi huku akibainisha kuwa mabadiliko ya kiwango cha timu yake kimechangiwa na kujengwa kwa morali ya wachezaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live