Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC wasikitishwa na matokeo

7d7bbb60a960cf827e5828ac2778ca44 Azam FC wasikitishwa na matokeo

Sun, 1 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA Msaidizi wa Azam FC Vivier Bahati amesema matokeo waliyopata katika michezo miwili iliyopita haijawafurahisha.

Azam FC imetoka kupata sare nyumbani ya bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa juzi usiku.

Hiyo ni sare ya kwanza wanaipata tangu kuanza kwa msimu huu, huku wakitoka kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar matokeo yaliyopunguza kasi yao ya ushindi.

Akizungumzia matokeo hayo baada ya mchezo dhidi ya JKT, Kocha Msaidizi Vivier Bahati alisema walikuwa na lengo la kupambana na kupata pointi tatu, lakini kadiri wanavyosogea mbele matokeo hayawafurahishi.

“Tulijaribu kutafuta nafasi ya kufunga, lengo letu lilikuwa kupata matokeo mazuri ila tumepata pointi moja hatuna namna naona ni mipango ya Mungu,”alisema.

Alisema matokeo hayo hayawafanyi wakate tamaa bali bado wako katika mapambano watajipanga upya kwa michezo ijayo ili kuhakikisha wanarejea katika kasi yao.

Matokeo hayo ni kama yatazidi kuwaweka kwenye presha kutoka kwa wapinzani wengine kama Simba na Yanga ambao nao wanatafuta nafasi ya uongozi.

Kwa upande wa Kocha wa JKT Mohamed Abdallah alisema anashukuru Mungu kwa sare waliyopata ingawa lengo lao lilikuwa kupata pointi tatu.

“Wenzetu walikuwa wanahitaji nafasi wameshindwa kuzitumia, sisi tumepata moja tumetumia. Timu zote mbili zimecheza vizuri, wameweza kushambulia na kutengeneza nafasi wameshindwa ila sisi tumepata moja tumetumia, ndio mchezo ulivyo,”alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz