Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC washindwe wenyewe tu!

Fei Mazoezi Azam Azam FC washindwe wenyewe tu!

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam msimu huu 2023/24 hawana sababu yoyote mwisho wa msimu kushindwa kufanya vizuri katika mashindano yote wanayoshiriki maana wamesajili wachezaji wazuri wamepata muda wa kutosha wa kufanya maandalizi nchini Tunisia.

Azam FC wamerejea nchini kwa kundi la kwanza wakiwa wachezaji sita maana wanarudi kwa mafungu mafungu wakitoka nchini Tunisia ambapo waliweka kambi ya mwezi mmoja na kucheza michezo mbalimbali ya kirafiki kwaajili ya kujiweka sawa na msimu mpya.

Wanalambalamba wamefanya usajili bora kuanzia kwa Kocha Mkuu Youssouph Dabo ambaye walimtambulisha mwishoni mwa msimu uliopita maanake kwa asilimia kubwa msimu huu ni mapendekezo yake na amepata muda wa kutosha na wachezaji wake pia wamefanya usajili bora wa baadhi ya wachezaji kama Feisal Salum, Sillah, Sidibe na wachezaji wengine wengi.

Bila kumsahau usajili wa dakika za mwisho kabisa wa Yannick Bangala kutoka Yanga kwahiyo tunatarajia ushindani mkubwa kutoka kwao katika kupambania ubingwa wa Ligi Kuu na makombe mengine wanayoshiriki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live