Kwa waliosomea Medicine (udaktari wa binadamu) watanielewa vizuri zaidi, lakini pia hata wale ambao hamjasomea udaktari ama unesi mtanielewa vizuri tu.
Magonjwa mengi huanza na dalili, mfano mtu mwenye High blood pressure (BP) huwa na symptoms kadhaa, hasa huumwa kichwa. Madaktari hushauri ukiumwa kichwa usinywe dawa ya kutibu kichwa kabla ya kupimwa kwa sababu unaweza kutibu kichwa kumbe una (BP).
Namaanisha nini? Azam FC wametibu kichwa badala ya kutibu (BP). Wametibu dalili badala ya tatizo. Tatizo kubwa la Azam msimu uliopita lilikuwa kwenye Centre-back na goalkicking. Wamesajili Viungo (2) Winger (1), mshambuliaji (1) na full-back (1).
Msimu wa 22 - 23
◉ Azam magoli ya kufunga— 55
◉ Azam magoli ya kufungwa — 29
◉ Simba magoli ya kufungwa — 17
◉ Yanga magoli ya kufungwa — 18
Ukitazama takwimu hizo utaona wazi kuwa, kufunga magoli haikuwa tatizo kubwa kwa Azam FC hata eneo la kiungo haikuwa shida ndio maana waliweza ku-dominate hata kwenye baadhi ya Míchezo mikubwa dhidi ya Simba na Yanga.
Watu watasema humuoni Bangala, si beki yule?! Ni kweli anaweza kucheza kama beki lakini wote ni mashahidi alipocheza eneo hilo akiwa Yanga, waliruhusu sana magoli kirahisi hadi Bacca alipo step up kikosini. Ikumbukwe, Bangala alikuwa MVP kutokana na kucheza eneo la kiungo na sio beki.
Azam wana Malick Ndoye ni beki mzuri lakini ana shida ya majeraha ya mara kwa mara, hakuhakikishii kucheza hata michezo (15) kwa msimu. Azam FC wamevaa suti mpya lakini ina tobo kwenye makalio bila kujua.