Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC walifeli hapa Kimataifa

IMG 20230825 WA0101 Azam FC walifeli hapa

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo ulianza kwa kasi mno kwa upande wa Azam FC huku wakiweza kuutawala Mchezo ndani ya zile dakika 15 za kipindi cha kwanza.

Bao la mapema la Iddy Nado liliweza kuongeza kasi ya ushambiliaji kabla ya Dube kushindilia bao la pili baada ya kumalizia pasi maridadi.

Azam FC ni kama waliona mechi wameshaimaliza baada ya kupata mabao 2 ya mapema ndani ya dakika 20, na kujikuta wanafanya kosa ambalo ndio lililowagharimu hadi sasa.

KIVIPI?

Viungo wa Azam FC walishindwa kufanya marking sahihi lwani walikuwa na idadi kubwa katika eneo la Bahiri ila pale wanapopoteza mpira wanashindwa kurudi Kwa wakati huku Bahiri wakitumia nafasi zilizoachwa na Azam kupiga pasi mpenyezo zilizofika kwa usahihi.

Walikuwa wachezaji zaidi ya 6 katika eneo lao huku Bahir wakiwa wawili tu lakini walishindwa kuzima shambulizi hilo lililopelekea bao kwa mpinzani wao.

Yule namba 11 wa Bahir, ile pasi yake iliyozaa bao ilikuwa superb. Katika utulivu wa hali ya juu akafanikiwa kupiga pasi katika ukuta wa watu zaidi ya 5 wa Azam FC mmmmh.

Iddi Nado hakika jana amekuwa na mchezo mzuri, nadhani anastaili kuwa nyota wa mchezo. Ameweza kutoa wakati mgumu kwa mabeki wa Bahir. Kwanza alikuwa na utulivu, ubunifu na kufanya maamuzi sahihi kila akifika kwenye box la Bahir.

Kwa nini kocha Dabo alimuacha Kipre Jr nje? Mchezo wa jana ulimuhutaji sana mchezaji huyu kwa jinsi anavyojua ku-drive mpira, zile movement zake zingekuwa na manufaa leo. Hata alivyoingia dakika chache za mwisho alionekna kubadilisha mchezo.

Bahir waliwaheshimu Azam FC sana kwani walionekana kuwaacha wauchezee mpira ila Wao wakiupata pasi mbili wameshafika langoni mwa Azam FC, kiufupi hawakutaka mambo mengi.

Siku zote mikwaju ya penalties hainaga mwenyewe lakini ukweli ni kuwa mlinda mlango wa Azam FC, Iddrisu alijitahidi kwa uwezo wake wote kuokoa penati 2 kati ya 6 lakini bahati haikuwa upande wao.

Azam FC Bado anamengi ya kujifunza juu ya Mashindano haya ya Kimataifa kwa kuwa huu ni mkosi sasa, kila kitu wanafanya kwa wakati lakini kutekeleza ndio tatizo.

FT; AZAM FC 2-1 BAHIR

AGG 3:3

PENALTIES AZAM 3- 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live