Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC wakubali yaishe Ubingwa Ligi Kuu Bara

Abdul Suleiman Sopu Ll Azam FC wakubali yaishe Ubingwa Ligi Kuu Bara

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam FC imejiondoa rasmi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu na kujiweka kwenye wakati mgumu kumaliza ndani ya mbili bora na sasa baadhi ya nyota wake wakikiri wana kibarua kumaliza msimu kwa heshima katika mechi zilizobaki.

Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Abdul Suleiman ‘Sopu’ amesema “Tumepoteza lengo la ubingwa tunahitaji nafasi ya tatu yenye ushindani kwa pointi tulizonazo tunahitaji 15 katika mechi tano zilizobaki, huku tukiwaombea Singida ichemshe,” alisema Sopu.

“Sisi kama wachezaji tunatakiwa kutumia muda huu kujitafakari ili kujiweka mazingira ya ushindani tukirudi tuanze upya kwa kukusanya pointi zote 15 kwenye mechi tano zilizobaki.”

Azam imebakiza mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting, Namungo, Coastal Union na Polisi Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live