Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC waitaka hatua ya Makundi Shirikisho Afrika

Hasheem Ibwe Nabi Azam FC waitaka hatua ya Makundi Shirikisho Afrika

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam FC wameondoka leo Agosti 18, 2023 kuelekea nchini Ethiopia kwa ajili kukipiga na Bahir Dar Kenema FC mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho Afrika, wamesema watapambana kuhakikisha wanafika hatua ya makundi.

Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema, wameondoka nchini kwenda kucheza mchezo huo utakaopigwa Jumapili Agosti 20, 2023 na malengo yao ni kushinda ili kujiweka vizuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar.

“Tumeondoka na wachezaji wote muhimu, hatuna injury Timu ina utimamu wa hali ya juu tunakwenda kupambana kwa ajili ya nchi yetu.

“Tumefanya maandalizi yote, tuna uhakika na tunachoenda kukifanya, tutapambana kuhakikisha Timu yetu kwanza inacheza group stage ya shirikisho, tukitoka hapo tutakwenda kwenye hatua nyingine ya mtoano,” alisema Ibwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live